Luke 3:1-8

Yohana Mbatizaji Aanza Kuhubiri

(Mathayo 3:1-12; Marko 1:1-8; Yohana 1:19-28)

1 aKatika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato akiwa mtawala wa Uyahudi, Herode akiwa mfalme wa Galilaya, Filipo ndugu yake akiwa mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania akiwa mfalme wa Abilene, 2 bnao Anasi na Kayafa wakiwa makuhani wakuu, neno la Mungu likamjia Yohana, mwana wa Zekaria huko jangwani. 3 cAkaenda katika nchi yote kandokando ya Mto Yordani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi. 4 dKama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya:

“Sauti ya mtu aliaye nyikani,
‘Itengenezeni njia ya Bwana,
yanyoosheni mapito yake.
5Kila bonde litajazwa,
kila mlima na kilima vitashushwa.
Njia zilizopinda zitanyooshwa,
na zilizoparuza zitasawazishwa.
6 eNao watu wote watauona
wokovu wa Mungu.’ ”
7 fYohana akauambia ule umati wa watu uliokuwa unakuja ili kubatizwa naye, “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja? 8 gBasi zaeni matunda yastahiliyo toba. Wala msianze kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Abrahamu, baba yetu.’ Kwa maana nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Abrahamu watoto kutoka mawe haya.
Copyright information for SwhNEN